Trump Abadilika Atangaza Tena Maongezi na Iran


Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kuwa Marekani inaendelea kufanya mazungumzo na Iran, lakini amesisitiza kuwa usitishaji wa mapigano umefikia mwisho.

Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii, Trump alisema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetuomba kuendelea na mazungumzo. Tumekubali ombi hilo, lakini Marekani imewaeleza wazi kwamba usitishaji wa mapigano umekwisha."

Kauli hiyo imekuja baada ya Marekani kushambulia maeneo kadhaa katika majimbo matano kusini mwa Iran, kufuatia mashambulizi dhidi ya meli zilizokuwa zikipita eneo hilo, Washington ikiilaumu Iran kwa mashambulizi hayo.

Aidha,maafisa wa Iran wamesema nchi hiyo ina haki ya kujibu mashambulizi yoyote yanayolenga miundombinu yake.

Idadi ya meli za kubeba mafuta zinazopita kila siku katika Mlango Bahari wa Hormuz imeonekana kupungua hii leo siku ya Ijumaa, baada ya Marekani na Iran kushambuliana na kuendeleza mabishano kuhusu nani anayedhibiti njia hiyo muhimu ya baharini.

Mashambulizi hayo yamezua tena wasiwasi kuhusu kuimarika kwa shughuli za usambazaji wa mafuta duniani na usafirishaji kwa njia ya bahari.

Hali hii inaonyesha jinsi makubaliano ya muda ya kusitisha mapigano yalivyo dhaifu huku Marekani na Iran zikiendelea kujadiliana ili kufikia makubaliano ya kudumu.

Post a Comment

0 Comments