Rais wa Marekani, Donald Trump, ametoa madai mapya kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, akisema kuwa nchi hiyo inamiliki akiba ya uranium iliyozikwa katika kina kikubwa sana chini ya ardhi kiasi kwamba hata mashine kubwa za kisasa za uchimbaji haziwezi kuifikia kwa urahisi.
Trump alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kuhusu uwezo wa Iran wa kuhifadhi malighafi za nyuklia, akisisitiza kuwa taarifa alizonazo zinaonyesha kuwa akiba hiyo imefichwa katika eneo lenye kina kikubwa kuliko uwezo wa vifaa vya kawaida vya uchimbaji.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Trump alisema Mohammed anasema kuna kitu kule (uranium) kinachohitaji kuchimbwa kwa kutumia koleo. Lakini majembe hayataweza kusaidia. Hata mashine kubwa zaidi duniani hazitaweza kusaidia.
Kwa mujibu wa Trump, taarifa hizo alizipata kutoka kwa afisa mmoja wa serikali ya Iran aliyemtaja kwa jina la Mohammed Alidai kuwa kufikia akiba hiyo kungehitaji operesheni maalumu kutokana na namna ilivyozikwa chini ya ardhi.
Hata hivyo, Rais huyo wa Marekani hakufafanua utambulisho kamili wa afisa huyo wala kutoa ushahidi unaothibitisha madai yake, hali iliyozua mjadala na maswali kuhusu mtu aliyekuwa akimrejelea.
Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya Mashariki ya Kati wameibua nadharia kwamba huenda Trump alikuwa akimaanisha Spika wa Bunge la Iran, . Hata hivyo, hadi sasa hakuna uthibitisho rasmi kutoka Marekani au Iran unaoonyesha kuwa ndiye aliyekuwa akizungumziwa katika kauli hiyo.
Kauli za Trump zinakuja wakati mvutano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran ukiendelea kuwa moja ya masuala nyeti katika siasa za kimataifa. Mataifa ya Magharibi yamekuwa yakieleza wasiwasi kuhusu shughuli za Iran za kurutubisha uranium, huku Iran ikiendelea kusisitiza kuwa mpango wake wa nyuklia unalenga matumizi ya amani na maendeleo ya nishati.
Hadi sasa, mamlaka za Iran hazijatoa tamko rasmi kujibu madai hayo ya Trump kuhusu uwepo wa akiba ya uranium iliyozikwa katika kina kikubwa cha ardhi.Rais wa Marekani, Donald Trump, ametoa madai mapya kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, akisema kuwa nchi hiyo inamiliki akiba ya uranium iliyozikwa katika kina kikubwa sana chini ya ardhi kiasi kwamba hata mashine kubwa za kisasa za uchimbaji haziwezi kuifikia kwa urahisi.
Trump alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kuhusu uwezo wa Iran wa kuhifadhi malighafi za nyuklia, akisisitiza kuwa taarifa alizonazo zinaonyesha kuwa akiba hiyo imefichwa katika eneo lenye kina kikubwa kuliko uwezo wa vifaa vya kawaida vya uchimbaji.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Trump alisema Mohammed anasema kuna kitu kule (uranium) kinachohitaji kuchimbwa kwa kutumia koleo. Lakini majembe hayataweza kusaidia. Hata mashine kubwa zaidi duniani hazitaweza kusaidia.
Kwa mujibu wa Trump, taarifa hizo alizipata kutoka kwa afisa mmoja wa serikali ya Iran aliyemtaja kwa jina la Mohammed Alidai kuwa kufikia akiba hiyo kungehitaji operesheni maalumu kutokana na namna ilivyozikwa chini ya ardhi.
Hata hivyo, Rais huyo wa Marekani hakufafanua utambulisho kamili wa afisa huyo wala kutoa ushahidi unaothibitisha madai yake, hali iliyozua mjadala na maswali kuhusu mtu aliyekuwa akimrejelea.
Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya Mashariki ya Kati wameibua nadharia kwamba huenda Trump alikuwa akimaanisha Spika wa Bunge la Iran, . Hata hivyo, hadi sasa hakuna uthibitisho rasmi kutoka Marekani au Iran unaoonyesha kuwa ndiye aliyekuwa akizungumziwa katika kauli hiyo.
Kauli za Trump zinakuja wakati mvutano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran ukiendelea kuwa moja ya masuala nyeti katika siasa za kimataifa. Mataifa ya Magharibi yamekuwa yakieleza wasiwasi kuhusu shughuli za Iran za kurutubisha uranium, huku Iran ikiendelea kusisitiza kuwa mpango wake wa nyuklia unalenga matumizi ya amani na maendeleo ya nishati.
Hadi sasa, mamlaka za Iran hazijatoa tamko rasmi kujibu madai hayo ya Trump kuhusu uwepo wa akiba ya uranium iliyozikwa katika kina kikubwa cha ardhi.
0 Comments