Msigwa Alipuka Tena Aanika Siri Nyingine Iliyomkimbiza CCM


Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa, ameanika siri iliyomfanya akimbie Chama Cha Mapinduzi (CCM), akidai kuwa alikuwa akipata wakati mgumu kiroho kutokana na kulazimika kusema uongo kwenye majukwaa ya siasa jambo lililokuwa likisuta dhamira yake ya uchungaji.

Mchungaji Msigwa alilipua bomu hilo jana Jumapili, Julai 5, 2026, wilayani Tarime mkoani Mara, wakati akihutubia maelfu ya waombolezaji waliokusanyika katika mazishi ya aliyekuwa dereva wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara (John Heche), marehemu Suez Dan Maradufu.

Mwanasiasa hiyo, aliyerejea CHADEMA miezi michache iliyopita, alieleza kuwa ukweli umekuwa bidhaa adimu sana nchini, hali iliyomfanya aone umuhimu wa kuchagua upande wa haki ili kuishi kwa misingi ya neno la Mungu badala ya kufuata matakwa ya kisiasa yaliyokuwa yakimtesa nafsi yake.

"Kusema ukweli kwenye nchi hii ni adimu. Nilipokuwa naitumia mikutano ilikuwa CCM, nilikuwa napata taabu kwa sababu inatakiwa useme uongo, na mimi ni mchungaji. Sasa nikiangalia Yesu anasema hivi na dunia inasema hivi, dhamira yangu ikanisuta. Kufanya kazi ndani ya CHADEMA katika mazingira haya ni kazi ngumu sana," alifunguka Mchungaji Msigwa. SOMA ZAIDI.

Post a Comment

0 Comments